Home Habari za michezo NO AISHI MANULA NO BENO KAKOLANYA NO PROBLEM…MANULA AMPONGEZA ALLY SALIMU

NO AISHI MANULA NO BENO KAKOLANYA NO PROBLEM…MANULA AMPONGEZA ALLY SALIMU

Habari za Simba SC

Golikipa namba moja wa Simba SC,Aishi Manula, amempongeza golikipa namba tatu wa timu hiyo kwa kuweza kuhimili mechi ya dabi na kuondoka na clean sheet.

Ally aliaminiwa kuanza leo na Kocha wa timu hiyo, Roberto Oliveira ‘Robetinho’ katika mechi ya dabi dhidi ya Yanga SC, na wekundu hao wa Msimbazi kuondoka na ushindi wa goli 2-0.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Aishi aliondoka maneno haya kama kumpongeza kijana huyo ambaye ni mara yake ya kwanza kuaminiwa katika mechi kubwa ya dabi

“No Aishi Manula, No Beno Kakolanya, no problem,” aliandika Aishi.
Simba wamecheza mchezo huo wa dabi wa 26 katika Ligi Kuu ya NBC na kufanikiwa kufikia alama 63 nyuma ya Yanga wanaoongoza Ligi wakiwa na alama 68.

Zimesalia mechi nne kwa kila timu kukamilisha msimu wa Ligi Kuu 2022/23.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA AWALETEA JEURI WAKONGWE WA SOKA...AMEIBUKA NA KUCHIMBA MKWARA MZITO