Home Uncategorized KUMEKUCHA NAMUNGO, BAADA YA KUIBOMOA ALLIANCE, SASA KUIBOMOA YANGA

KUMEKUCHA NAMUNGO, BAADA YA KUIBOMOA ALLIANCE, SASA KUIBOMOA YANGA

BAADA ya Namungo FC kumsajili mshambuliaji wa Alliance FC, Bigirimana Blaise kwa kandarasi ya mwaka mmoja imeelezwa kuwa wanaiwinda saini ya mlinda mlango wa Yanga, Ramadhan Kabwili ili aongeze nguvu kwenye kikosi chao.

Kabwili kwa sasa mkataba wake na Yanga imeelezwa umemalizika na bado hajaitwa mezani kuzungumzia ishu yake hali inayompa nafasi ya kuwa huru kuzungumza na timu yoyote inayomhitaji kwa sasa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Namungo, Kidamba Namlia amesema kuwa uwezo wa kikosi cha Namungo kwa sasa ni kusajili wachezaji wenye uzoefu wa kutosha hivyo hawaoni taabu kuzungumza na mlinda mlango wa Yanga, Kabwili.

“Ripoti tunayo na tunahitaji kusajili wachezaji wenye nguvu ya kutupa matokeo hatuna tatizo na aina ya wale tutakaowasajili hivyo hata Kabwili naye ni mlinda mlango imara tunao uwezo wa kumongea na uongozi endapo atahitajika,” amesema Namlia.

SOMA NA HII  NYONI: SIMBA ITAIFUNGA FC PLATINUM