Home Uncategorized BEKI SIMBA KUIBUKIA UTURUKI

BEKI SIMBA KUIBUKIA UTURUKI


 ABDI Banda, nyota wa Klabu ya Highlands Park ya Afrika Kusini anasubiri ofa ya timu  moja ya nchini Uturuki baada ya kurejea Bongo kutokana na timu hiyo aliyokuwa anaitumikia awali kupata bosi mpya jambo lilifanya mfumo kubadilika.

Beki huyo mzawa ambaye amecheza pia Baroka FC ameweka wazi kuwa kuna mawasiliano ya pande mbili hivyo mambo yakienda sawa anaweza kusepa.

Msimu wa 2014-17 alicheza ndani ya Klabu ya Simba ambapo aliibuka huko akitokea Klabu ya Coastal Union. 

Ndani ya Baroka FC alicheza jumla ya mechi 41 na alitupia mabao manne.Kwenye timu yake ya Highlands Park alicheza jumla ya mechi 4.

“Kuna mawasiliano ya pande mbili kwa sasa kati ya meneja wangu na mabosi wa nchini Uturuki hivyo mambo yakiwa sawa nitajua wapi nitakapokwenda kucheza,” .

SOMA NA HII  HAYA HAPA MAJUKUMU YA SENZO NDANI YA YANGA, KIBALI CHAKE BADO KIPO SIMBA