Home Uncategorized KMC SASA KUSAJILI WA KIMATAIFA

KMC SASA KUSAJILI WA KIMATAIFA


BAADA ya kikosi cha Manispaa ya Kinondoni, KMC kupata zali la kushiriki michuano ya kimataifa msimu wa mwaka 2019/20 uongozi umepania kuboresha kikosi kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ya kimataifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema kuwa kwa sasa watabadilisha mtindo wa kusajili kutokana na kupata nafasi hiyo hivyo lazima wafanye kitu cha utofauti.

“Ni nafasi yetu sasa kupeperusha Bendera kimataifa, hatutaweza kufanya vizuri kama tutasajili wachezaji wa kawaida ni lazima tuongeze nguvu kubwa kwa kusajili wachezaji wenye uzoefu, hivyo tutaboresha usajili wetu na kufanya usajili wa maana kwa ajili ya michuano ya kimataifa,” amesema Binde.

SOMA NA HII  SIMBA QUEENS YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA YANGA PRINCESS