Home Uncategorized ZINEDINE ATAMANI MESSI ASIONDOKE BARCELONA

ZINEDINE ATAMANI MESSI ASIONDOKE BARCELONA

ZINEDINE Zidane,  Kocha Mkuu wa Real Madrid amesema kuwa anatamani kumuona nyota wa kikosi cha Barcelona Lionel Messi anabaki ndani ya kikosi hicho ili kuongeza ushindani ndani ya La Liga. 

Mkataba wa Messi unameguka Juni 20,2021 huku ikitajwa kuwa yupo kwenye mpango wa kusepa ndani ya kikosi hicho. 

Haijafahamika kwamba iwapo Messi mwenye miaka 33 atasepa ndani ya klabu hiyo ataibukia wapi ila Manchester United ilikuwa inatajwa kuiwinda saini yake.

Zidane amesema kuwa anatamani kumuona Messi, mchezaji bora wa dunia mara sita, (Ballon d’Or) akiendelea kuitumikia Barcelona ili kuleta ushindani hasa kwa upande wao Real Madrid.

“Sijui kitu gani kitatokea mbeleni ila tuna matumaini atakuwepo ndani ya ligi hii,”.

SOMA NA HII  GWAMBINA FC: TULIKWAMA DAR, TUKAIBUKIA MWANZA