Home Uncategorized WACHEZAJI WA SIMBA WAFUNGUKA A-Z WALIVYOPOTEZA FAINAL YA CAF 1993..WAMTAJA DEWJI NA...

WACHEZAJI WA SIMBA WAFUNGUKA A-Z WALIVYOPOTEZA FAINAL YA CAF 1993..WAMTAJA DEWJI NA TFF

LICHA ya miaka 27 kupita, kovu la kipigo cha mabao 2-0 cha Simba dhidi ya Stella Abdijan ya Ivory Coast kwenye fainali ya CAF halijafutika kwa nyota wa Simba ambao wamefafanua tuhuma za kuuza mechi na wachezaji kuzichapa wenyewe kwa wenyewe katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Simba iliruhusu kipigo cha mabao 2-0 baada ya suluhu ugenini nchini Ivory Coast, mechi ambayo imeendelea kubaki kwenye kumbukumbu za nyota wa Simba waliocheza mwaka 1993.

Wekundu wa Msimbazi walipoteza ahadi ya kununuliwa magari makubwa ya mizigo aina ya KIA kwa kila mchezaji, iliyotolewa na aliyekuwa mfadhili wao, Azim Dewji.

Kipa aliyedaka katika mchezo huo, Mohammed Mwameja anasema kipigo hicho hakijawahi kufutika kichwani mwake, na mechi hiyo imekuwa mechi chungu katika historia yake ya soka.

“Huwa nikiikumbuka ile mechi napata uchungu, ni muda mrefu umepita lakini maumivu yake hayajawahi kufutika kwangu,” alisema kipa huyo nyota wa zamani wa Simba na Taifa Stars.

Alisema leo hii Simba ingekuwa na jambo la kutambia mbele ya watani wao Yanga, lakini haikuwa bahati yao huku akisisisitiza kuwa hakuna ukweli wa tuhuma walizopewa kwamba waliuza mechi hiyo.

“Tulijiamini kupita kiasi hasa baada ya kusuluhu ugenini, tulijua tumeshashinda nyumbani, hicho ndicho kilituponza, hakuna mechi inaniumiza kama ile,” alisema Mwameja ambaye ni miongoni mwa makipa bora kwenye historia ya Tanzania.

Malota Soma aliyecheza namba 10 katika mchezo huo alisema; “Watu wa FAT (sasa TFF) na Serikali walituvuruga, ilikuwa ni shamra shamra hata kabla ya ubingwa, kambi yetu Zanzibar haikuwa na utulivu, ilikuwa ni vurugu tu, hata mazoezi wachezaji waliokuwa kambini walikuwa nusu ya timu hadi dakika za mwishoni.”

“Hakuna mchezaji aliyepigana, baada ya mechi kila mmoja aliondoka na kambi ilivunjwa,” alisema.

Winga wa kushoto katika mechi hiyo, Thomas Kipese alisema maandalizi baada ya mechi ya ugenini ndiyo yaliwaponza.

“Mengi yalizungumzwa wakati ule na mpaka sasa wapo watu wanaoamini wachezaji waliuza mechi, lakini asikwambie mtu, hata sisi tulikuwa na shauku ya ubingwa, leo hii ingekuwa historia kubwa mno kwetu, basi bahati haikuwa upande wetu,” alisema.

SOMA NA HII  BREAKING:MORRISON WA YANGA ASAINI SIMBA