Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YAO YA LIGI…GEITA GOLD WAICHIMBA MKWARA WA ‘KISUKUMA’ SIMBA…

KUELEKEA MECHI YAO YA LIGI…GEITA GOLD WAICHIMBA MKWARA WA ‘KISUKUMA’ SIMBA…

Geita Gold FC

Simba imetua mkoani Mwanza kwa ajili ya kucheza mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita.

Wekundu hao wa Msimbazi ambao walimaliza mzunguko wa kwanza wakiwa katika nafasi ya tatu wanataka kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo ya mzunguko wa pili, ili kutimiza malengo yao ambayo waliyatangaza mwanzoni mwa msimu huu ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Hata hivyo, timu hiyo ambayo itacheza michezo mitatu Kanda ya Ziwa kabla haijarejea Dar es Salaam, imepigwa mkwara mzito na Geita Gold, kuelekea mchezo wao wa Jumapili Ijayo kwenye Dimba la CCM Kirumba, Mwanza.

Kocha msaidizi wa timu ya Geita, Mathias Wadiba, amesema kuwa hawana hofu na Simba kwa kuwa wote wapo daraja moja wakicheza Ligi Kuu pamoja na kwamba wanawaheshimu.

“Tunawaheshimu Simba, lakini hatuna hofu nao kwa kuwa wote tunacheza ligi moja, tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo na tunaamini kuwa tutafanya vizuri,” alisema kocha huyo.

Wakati Simba wakiwa nafasi ya tatu na pointi 34, lakini wakiwa vinara wa kufunga mabao baada ya kufunga 31, lakini wakiwa pia wanashika nafasi ya kwanza kwa kufungwa mabao machache baada ya kuruhusu saba tu huku Geita wakiwa nafasi ya tano baada ya kukusanya pointi 22 kwenye michezo 35.

Huu unatajwa kuwa mmoja kati ya michezo mizuri kutokana na upinzani ambao Simba wamekuwa wakikutana nao kila wanapokwenda mkoani kwenye michezo ya ligi kuu

SOMA NA HII  PAMOJA NA YANGA KUCHOONGA SANA SAFARI HII..SIMBA WAIHENYESHA KWA MIAKA 10...ISHU IKO HIVI...