Home Habari za michezo KUELEKEA UCHAGUZI MKUU SIMBA…KABURU NJIA NYEUPEEE…KAZI ILIYOBAKI NI HII…

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU SIMBA…KABURU NJIA NYEUPEEE…KAZI ILIYOBAKI NI HII…

Habari za simba

Aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ juzi alijitosa kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Januari 29, mwakani, huku ikifafanuliwa kuwa ni mtu mwenye haki ya kugombea nafasi yoyote kwa mujibu ya Katiba.

Kaburu alishika nafasi hiyo kabla ya kupata matatizo ya kisheria wakidaiwa kuwa na matumizi mabaya ya ofisi pamoja na aliyekuwa Rais wa Simba, Evans Aveva, ambapo alikaa mahabusu kwa muda mrefu hivyo kuwa nje ya soka.

Hivi karibuni, Kaburu ambaye siku ya hukumu ya kesi yao kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alionekana kutokuwa na hatia, hivyo kuachwa huru huku Aveva akikutwa na hatia na kufungwa kifungo cha nje kwa miezi sita, amekuwa akionekana kwenye shughuli mbalimbali za klabu hiyo ikiwemo kuwa katika kamati ya ujenzi ya Uwanja wa Mo Arena uliopo Bunju.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi huo, Boniface Lihamwike alifafanua kuwa, Kaburu ana haki ya kugombea kikatiba kwani Mahakama haikumkuta na kosa lolote hivyo anahesabika kama mtu ambaye hajawahi kushitakiwa kwa kosa lolote lile.

“Sheria ipo wazi, Kaburu hakuhukumiwa na mahakama haikumkuta na kosa lolote, hata kama alikaa mahabusu lakini Mahakama haikumhukumu, hivyo anahesabika hajawahi kushitakiwa na kwa lolote lile na ana sifa zote za kugombea kwenye uchaguzi huu na kufanya shughuli zozote zile.

“Hivyo kama mwenyekiti, sina tatizo na Kaburu kuchukua fomu na taratibu zote za uchaguzi zitafanyika kama tulivyopanga, siku ya mwisho wapiga kura ndiyo watakaoamua,” alisema Lihamwike ambaye ni Hakimu Mkazi Mahakama ya Babati, Manyara

Kwa upande wa Kaburu alisema; Ni kweli nimechukua fomu na nitairudisha, mengine yatafuata baada ya taratibu zote zilizowekwa na wasimamizi wa uchaguzi.”

Katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti, wagombea wengine waliochukua fomu juzi ni Yusuph Omar Yenga na Injinia Rashid Khamis.

Nafasi ya ujumbe waliochukuwa fomu hadi sasa ni Iddy Noor Kajuna, Abubakari Zebo, Abdallah Rashi Mgomba, Hawa Mwaifunga, Laurian Mganga, Elisony Edward Mweladzi na Lameck Lawrance huku mwisho wa kuchukua fomu hizo ni Desemba 19, mwaka huu

SOMA NA HII  ALICHOSEMA KAGERE BAADA YA KUSHUKA KWENYE JUKWAA LA SIMBA...AFUNGUKA MENGINE MAPYA USIYOYAJUA...