Home Habari za michezo BAADA YA DIRISHA LA USAJILI KUFUNGULIWA LEO…YANGA KAMA HAWATAKI VILEE…ONA ALICHOSEMA HERSI…

BAADA YA DIRISHA LA USAJILI KUFUNGULIWA LEO…YANGA KAMA HAWATAKI VILEE…ONA ALICHOSEMA HERSI…

Habari za Yanga

Wakati Dirisha Dogo la Usajili likifunguliwa Rasmi leo Ijumaa (Desemba 16), Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans wameweka wazi kuingia sokoni kusaka Wachezaji.

YoungAfricans inayotetea Taji la Ligi Kuu pamoja na Kushiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, imekuwa ikitajwa kuwa kwenye mazungumzo na baadhi ya Wachezaji ambao huenda wakasajiliwa katika kipindi hiki.

Rais wa Young Africans Injinia Hersi Said amesema ni kweli wataingia sokoni ili kufanya usajili wa Wachezaji kadhaa ambao wataongeza nguvu katika kikosi chao.

Hata hivyo Hersi hakutaka kuwa wazi kwa kueleza ni maeneo gani katika kikosi chao watayaongezea nguvu, na Wachezaji ambao wanawawania ili kuwasajili katika Dirisha Dogo.

“Lazima tuboreshe kikosi, hiyo ni lazima! Lazima tuongeze wachezaji wenye uwezo mkubwa ambao watatusaidia kufika mbali ziadi. Nani na kwa vipi, tuwe tayari kwa hilo. Naamini mashindano ya kimataifa ni sehemu nzuri kwa Yanga kuanza kuweka muhuri wake.” amesema Hersi Said

Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikifikisha alama 38 baada ya kucheza michezo 15 ya Duru la Kwanza, huku kesho Jumamosi (Desemba 17) ikitarajia kucheza dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Mzunguuko wa 16.

Pia Young Africans imepangwa Kundi D katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika na Mabingwa mara tano wa Bara hilo TP Mazembe (DR Congo), US Monastir (Tunisia) na Real Bamako (Guinea).

SOMA NA HII  YANGA NAO WAONJA LADHA YA USHINDI