Home Uncategorized MCHEZAJI SIMBA AELEKEA MOROCCO

MCHEZAJI SIMBA AELEKEA MOROCCO


Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC na Napsa Stars ya Zambia, Laudit Mavugo amejiunga na klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco anayocheza Mshambuliaji wa Tanzania Saimon Msuva.

Baada ya mazungumzo mrefu, dili hilo limekamilika na Mavugo sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji wa timu hiyo kwa msimu huu.

Mavugo aliwahi kucheza Simba misimu kadhaa iliyopita lakini baadaye akaachwa baada ya kukosa nafasi ndani ya wekundu wa Msimbazi.

Ikumbukwe kabla hajatua Simba, mabosi wa klabu hiyo walihaha kwa takribani misimu mitatu kupata saini yake lakini baadaye akaachwa kutokana na kiwango chake kuwa dhaifu.
SOMA NA HII  GAMONDI AWAPA ANGALIZO HILI MASTAA YANGA