Home Azam FC ISHU YA MANULA KURUDI CHAMAZI..JEMEDARI AWAIBIA SIRI MABOSI AZAM…”THAMANI YAKE NI BIL...

ISHU YA MANULA KURUDI CHAMAZI..JEMEDARI AWAIBIA SIRI MABOSI AZAM…”THAMANI YAKE NI BIL 2.3″..

Tetesi za Usajili Simba

Kipa wa Simba SC, Aishi Manula bado ana mkataba wa miaka miwili na Simba SC kwa sasa hakuna klabu iliyomsajili au kuhitaji huduma ya kipa huyo bora kutoka NBC Premier league.

Huku meneja wa golikipa Huyo, Jemedari Said amesema kuwa Manula bado ana mkataba wa miaka miwili na Simba ambao utaisha June 2025 kama kuna klabu yoyote inayomtaka Manula kuna kipengele cha kutoa dola milioni 1 (zaidi ya bilioni 2.3 za Kitanzania) ili kuvunja m kataba wake na Simba SC.

Manula bado anauguza Jeraha lake alilo lipata Hivi karibuni na klabu ya Simba sc inajiandaa kumpeleka Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi ya majeraha yake.

“Mchezaji ni wa klabu kwa hiyo mwenye jukumu la kumtibu ni klabu yake ya Simba. Huwezi kuwahoji kwa nini hawamtibu lakini najua watamtibu tu. Tayari taratibu zimeshafanyika na muda si mrefu atapelekwa kwenye matibabu wiki hii.

“Amepelekwa Muhimbili, ikaonekana kuna damu imevuja kwa ndani na madaktari wakabaini msuli umekatika kwa hiyo anahitaji upasuaji ambapo utafanyika nje ya nchi.

“Manula amesaini kataba mpya Simba mwaka jana, tena wa miaka mitatu, kwenye mkataba wake kuna kipengele cha kwamba iwapo kuna timu inamhitaji basi itoe dola milioni 1 (zaidi ya Tsh bilioni 2.3). Kwa hiyo kama kuna timu inamtaka waende Simba pale na pesa hiyo wala hakuna maneno.

“Sisi hatujapata chochote (maombi ya kumnunua) na Manula hamdai chochote Simba, pesa yake ya usajili alipewa yote na mshahara analipwa kila mwezi,” amesema Jemedari.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AFUNGUKA HAYA KUHUSU LUIS MIQUISSONE