Home news KISA CAF….SIMBA NA YANGA KUANZA KUPISHANA ANGANI KAMA ‘NJIWA’…MCHONGO MZIMA UKO HIVI…

KISA CAF….SIMBA NA YANGA KUANZA KUPISHANA ANGANI KAMA ‘NJIWA’…MCHONGO MZIMA UKO HIVI…

Habari za Simba na Yanga

Wawakilishi wa Tanzania Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika, Simba na Yanga zina mlima mrefu wa kuupanda kuhakikisha zinatinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo makubwa ngazi ya klabu huku wakitembea jumla ya kilomita .

Hivyo ndiyo unaweza kusema kutokana na kilometa watakazo zitumia kufuata pointi tisa ugenini zitazunguka mataifa matatu tofauti kwa usafiri wa ndege.

Simba ambayo inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ipo kundi ‘C’ ikiwa na timu za Horoya (Guinea), Vipers (Uganda) na Raja Casablanca ya Morocco, wakati Yanga wao wakiwa wamepangwa D wakiwa na TP Mazembe, Bamako ya Mali na Monastir ya Tunisia.

Kutokana na umbali wa nchi hizo Simba inaonekana kuwa na umbali zaidi wa kusafiri kwa ndege tofauti na wapinzani wao Yanga kwani itawalazimu kutumia Kilomita 37, 712 sawa na umbali wa safari za nchi zote tatu.

Mechi ya kwanza Simba itacheza ugenini dhidi ya Horoya nchini Guinea Februari 10, mwakani umbali kutokea, Dar es Salaam hadi Guinea itatumia Kilomita 16,408 umbali wa kwenda na kurudi ikitumia shirika la ndege ya Ethiopia ambalo ndiyo linaonekana kuwa rahisi sana kwenda huko.

Kama Simba italazimika kuchukua shirika la ndege lingine au ikitumia ndege ya kukodi hadi nchini humo kilomita hizo zinaweza zikapungua au kuongezeka.

Mfano, Simba wakitumia Shirika la Emirates watatakiwa kwenda hadi Dubai na kurejea tena Afrika ili kwenda Guinea ambapo kimahesabu safari hiyo itakuwa ndefu zaidi. Simba itakuwa na Kilomita nyingine 2,652 kufukuzia pointi tatu Uganda kwa ndege watakapoifuata Vipers Februari 24.

Hapa hakutakuwa na mzunguko mrefu kwani inaweza kwenda na shirika la ndege la nchi hiyo moja kwa moja kutua Kampala au la hapa nchini Tanzania.

Baada ya hapo itacheza mechi nyingine ugenini dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco Machi 31, itatumia kilomita 18,652, kutoka Dar hadi kufika nchini humo kama itakuwa imetumia shirika la ndege ya Ethiopia.

Ikitokea Simba ikaenda na shirika la ndege lingine au kutumia yake binafsi kwa maana ya kukodi kama ilivyofanya kwenye safari ya Angola kucheza na Primiero de Agosto inaweza kuwa njiani muda mfupi au mrefu tofauti na kilomita itakazotumia na Ethiopia.

Wakati Simba wakiwa na mlima huo mrefu watani zao Yanga, ambao wapo Kombe la Shirikisho wao watakuwa na kilomita chache sana, watatumia kilomita 19,998 kusaka pointi tisa ugenini wakisaka nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga ipo kundi ‘D’ dhidi ya vigogo wa soka la Afrika TP Mazembe (Congo), US Monastir (Tunisia) na Real Bamako kutokea Mali.

Yanga itaanzia ugenini Februari 12, Tunisia dhidi ya US Monastir ikitumia usafiri wa ndege shirika la Ethiopia itatumia kilomita 15,990 kutokea Dar hadi nchini huku kama ikibadilisha shirika la ndege inaweza kuwa zaidi ya hapo.

Kama unakumbuka mechi ya mtoano kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika, Yanga ilipata ushindi wa bao 1-0, ugenini Tunisia dhidi ya Club Africain na msafara wa timu hiyo ulitumia shirika la ndege ya Emirates ulienda hadi Dubai kisha kurudi Tunisia, kama itakuwa hivi tena inamaana pointi tatu hapa zitakula kilomita nyingi zaidi.

Februari 26, Yanga itaanza safari ya kuifuata Real Bamako itatumia kilomita 1,056, itatokea Dar hadi Ethiopia na kupanda ndege ya moja kwa moja hadi Mali.

Aprili 2, Yanga itakuwa ugenini kuvaana na TP Mazembe safari ya kwenda na kurudi kuwafuata wapinzani wao itakuwa kilomita 2952 kwa shirika la ndege la Ethiopia kwani itawalazima kupitia nchini Ethiopia kwanza.

SOMA NA HII  'JUJU' ZA MBOMBO ZAMPAGAWISHA ONGALA AZAM FC...HASIKII WALA HAAMBILIKI KWAKE...