Home Habari za michezo BAADA YA KIMYA KIREFU….MZEE KILOMONI AIBUKA NA HILI JIPYA KWA SIMBA….AMPA MAAGIZO...

BAADA YA KIMYA KIREFU….MZEE KILOMONI AIBUKA NA HILI JIPYA KWA SIMBA….AMPA MAAGIZO MO DEWJI…

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Klabu ya Simba, Hamis Kilomoni amesema uongozi wa klabu hiyo unatakiwa kuingia mfukoni na kusajili washambuliaji wawili wa maana ili timu hiyo itishe kimataifa.

Kilomoni alisema amekuwa akifuatilia mechi za Simba lakini bado ana wasiwasi na ubora wa washambuliaji wa Simba kwa jicho la kimataifa kwani wengi hawachezi anavyodai vizuri.

Simba ina washambuliaji wengi akiwemo John Bocco, Habib Kyombo na wakati mwingine humtumia Moses Phiri, lakini wamekuwa wakilalamikiwa kwa kushindwa kuonyesha kiwango.

Phiri ndiye amekuwa bora zaidi msimu huu akiwa amefunga mabao 10 kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa analingana kwa mabao na Fiston Mayele wa Yanga.

Kilomon ambaye amewahi kuwa mchezaji wa Simba alisema washambuliaji wa Simba wamekuwa wakicheza kivivu hivyo wanatakiwa kujitathimini ili kuipa mafanikio timu hiyo.

“Huwa naangalia mechi za Simba lakini watu wa mbele pale wananiudhi wakati mwingine kwani hawachezi kwa nguvu, hata sisi tulivyokuwa tunacheza enzi zetu tunawazidi kwa ubora.

“Mtu anapokuwa eneo la hatari au nje kidogo, anapiga mpira utafikiri mtoto mdogo, utafungaje kwa namna hiyo, lazima mshambuliaji ukipiga shuti liwe na uzito ili hata kama likigonga mwamba wa goli unatikisika, lakini hawa sijui hawali chakula sawasawa sielewi, “alisema.

“wanakwenda hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika lazima wawe na watu wa kazi ili timu ipate matokeo mazuri.

Kilomoni alisema eneo la beki hakuna tatizo kabisa kwani kwa sasa pametulia na hana shaka nalo.

SOMA NA HII  NYOTA WAWILI SIMBA WAACHWA JUMLAJUMLA