Home Uncategorized HERITIER MAKAMBO AINGIA ANGA ZA YANGA TENA

HERITIER MAKAMBO AINGIA ANGA ZA YANGA TENA


HERITIER Makambo, nyota wa zamani wa Yanga inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za kurejea ndani ya kikosi hicho kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji.

Makambo msimu wa 2018/19 alikuwa akiwajaza mashabiki wa Yanga kila anapofunga jambo lililompa umaarufu na alicheza msimu mmoja na kutimkia zake Horoya FC.

Akiwa Yanga Makambo alitupia mabao 17 ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ni mfungaji wa tatu ambapo nafasi ya kwanza ilikuwa kwa Meddie Kagere mwenye mabao 23 na ya pili ilikuwa kwa mzawa Salim Aiyee aliyetupia mabao 18.

Luc Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga alisema kuwa anahitaji kupata mshambuliaji halisi atakayesaidiana na Ditram Nchimbi na David Molinga ndani ya Yanga.

Habari zinaeleza kuwa anayefuata kutua hapo ni Makambo huku uongozi wa Yanga ukiwataka mashabiki watulie.

SOMA NA HII  BOCCO AACHA BALAA KWA LIPULI YA DIDA NAMNA HII