Home Uncategorized BOCCO AACHA BALAA KWA LIPULI YA DIDA NAMNA HII

BOCCO AACHA BALAA KWA LIPULI YA DIDA NAMNA HII


JOHN Bocco, nahodha wa Simba ameacha balaa kwa Lipuli baada ya kuwafunga bao kwenye ushindi walioupata Simba mbele ya Lipuli kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Februari 15 Uwanja wa Samora kwa kumtungua mlinda mlango Deogratius Munish ‘Dida’ kwa  shuti la guu la kushoto.
Tangu Simba ishinde mbele ya Lipuli kwa bao 1-0 mpaka leo, Lipuli imekumbwa na balaa la kuyeyusha pointi tatu kwenye mechi wanazocheza za ligi huku Dida akiongeza idadi ya mabao ya kuokota nyavuni.
Ikiwa Lipuli imecheza mechi tatu ambazo ni sawa na dakika 270 imeyeyusha pointi tisa ilizokuwa ikisaka na kukubali kuokota mabao sita langoni kwa Dida huku wao wakifunga mabao mawili pekee.
Februari 18 Lipuli ikiwa Uwanja wa Sokoine ilikubali kichapo cha mabao 2-1.Februari 23 ilichapwa mabao 2-0 na Prisons Uwanja wa Samora na Februari 29 ikiwa Samora ilikubali kuchapwa mabao 2-1 na Namungo FC.
Dida amejiunga na Lipuli kwenye usajili wa dirisha dogo akiwa mchezaji huru baada ya kumalizana na Simba, aliwahi kuidakia pia Yanga na anashikilia rekodi ya kuwa golikipa aliyefunga goli ndani ya ligi msimu huu.
SOMA NA HII  KATWILA: TUTAYAFANYIA KAZI MAKOSA YETU