Home Uncategorized OFISA HABARI WA SIMBA ATINGA MAKAO MAKUU YA YANGA, HIKI HAPA AMESEMA

OFISA HABARI WA SIMBA ATINGA MAKAO MAKUU YA YANGA, HIKI HAPA AMESEMA


ANAANDIKA Haji Manara,kupitia ukurasa wake wa Instagram Ofisa Habari wa Simba:-Heri neno kavu na utulivu kuliko karamu ya Mfalme na machafuko ‘Bible’.


“Nilikwenda mwenyewe mchana huu klabuni Yanga,bahati mbaya sana sikuwakuta viongozi wa klabu. Wazee niliowakuta nje baada ya kuwaeleza nimekuja kukabidhi pesa za masimango walinisihi sana nisifanye hivyo na wakaniambia yule ni mgeni hapa mjini na hajui tamaduni zetu na kuniomba nisirejeshe hata thumuni.


 Nimefundishwa kuwatii wazee, na ntarejea kwa Wanasimba walionikabidhi pesa zao,busara itawashauri tupeleke hospitali kwa wagonjwa wasiojiweza,ikiwapendeza tutafanya hvyo!


Kwetu nimefundishwa uungwana,kwetu nimepata malezi bora,kwetu wazazi wangu walinijaza na jeuri ya kutokubali kuonewa wala kunyanyaswa. halaf mm sijatoka Mbwinde,,hilo ni Muhimu sana na ndio maana naweza kuwa Msemaji pekee naweza kwenda klabu nyingine tena mchana kweupeeeee.

SOMA NA HII  HUYO PILATO WA YANGA NA SIMBA NOMA, YANGA ILILIA PENALTI, SIMBA KADI NYEKUNDU