Home news INJINIA HERSI AFUNGUKA MAPYA KWENYE MSIBA WA SONSO…ADAI HAJAFANYANAYE KAZI..AGUSIA NIDHAMU YAKE…

INJINIA HERSI AFUNGUKA MAPYA KWENYE MSIBA WA SONSO…ADAI HAJAFANYANAYE KAZI..AGUSIA NIDHAMU YAKE…


Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga Mhandisi Hersi Said amesema msiba wa beki huyo utabaki kuwa kidonda kwa klabu ya Yanga kutokana na umahiri wa marehemu.

Hersi ambaye aliunaga na kikosi cha Yanga katika mazishi ya beki wao huyo wa zamani amemuelezea Sonso kwamba alikuwa beki mwenye kujituma na kuwahamasisha wenzao.

“Bahati mbaya sikufanya kazi sana na Sonso nilimkuta akiwa muda wake wa mwisho ndani ya Yanga nakumbuka wakati huo timu ilikuwa chini ya makocha Luc Eymael na Charles Mkwasa,”amesema Hersi.

“Muda huo mdogo Sonso alikuwa ni beki wa kazi hasa,nilipenda alivyokuwa anawahamasisha wenzake kupambana na hata alipokuwa uwanjani alionyesha juhudi zake kwa vitendo.

Aidha Hersi ameongeza kwamba nidhamu ya Sonso ilikuwa ni nguzo muhimu wakati wa uhai wake ambapo hata alipoondoka klabuni hapo bado hakuonyesha kitu chochote kibaya.

“Kikubwa zaidi nidhamu ya Sonso ilikuwa ya kiwango kikubwa na nafikiri umati huu mkubwa uliojitokeza katika msiba huu unatosha kutoa kielelezo kwamba marehemu alikuwa mtu wa aina gani.”

Katika hatua nyingine Hersi ambaye pia ni mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM walitoa ubani wa Sh2 miliioni huku Yanga wakitoa Sh1 milioni.

SOMA NA HII  RASMI...MAYELE AKABIDHIWA DUME LA NG'OMBE NA SHABIKI WA MOROGORO ...LAFUGWA KLABUNI..