Home news RASMI…MAYELE AKABIDHIWA DUME LA NG’OMBE NA SHABIKI WA MOROGORO …LAFUGWA KLABUNI..

RASMI…MAYELE AKABIDHIWA DUME LA NG’OMBE NA SHABIKI WA MOROGORO …LAFUGWA KLABUNI..


Shabiki wa Klabu ya Young Africans Peter Kanduru ametimiza ahadi yake kwa kumzawadia Ng’ombe Mshambuliaji hatari wa klabu hiyo kwa sasa, Fiston Kalala Mayele.

Kanduru alitoa ahadi hiyo baada ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa Manungu, Turiani Mkoani Morogoro Februari 23.

Katika mchezo huo Mayele aliifungia Young Africans bao la pili, huku Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Saido Ntibazonkiza akifunga bao la kwanza.

Mapema Leo Jumatatu (Machi 14), Kanduru alifika Makao Makuu ya klabu ya Young Africans akiwa na Ng’ombe huyo na kumkabidhi Mshambuliaji Mayele.

Mayele ndio anaongoza katika upachikaji mabao kwenye Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22 akifunga mabao 10, sawa na Mshambuliaji wa Namungo FC Reliant Lusajo.

SOMA NA HII  ISHU YA USAJILI YANGA...MANARA AANIKA HADHARANI WAKIMATAIFA WATAKAO SAJILIWA...AMTAJA MORRISON KIMAFUMBO...