Home news KAULI YA RAGE KUIFANANISHA LIGI KUU YA NBC NA ‘LIGI YA...

KAULI YA RAGE KUIFANANISHA LIGI KUU YA NBC NA ‘LIGI YA MBUZI’..YAMTOKEA PUANI…’ALIPULIWA’ NA MBUNGE…


Mbunge wa Jimbo la Makete na Mwanachama wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Festo Richard Sanga, ameonesha kukerwa na kauli iliyotolewa na mdau wa soka nchini Ismail Aden Rage, alipohojiwa na vyombo vya habari jana Jumapili (Machi 13).

Rage ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Simba SC alitoa kauli ya kuidharau Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuiita Ligi ya Mbuzi, jambo ambalo limepingwa vikali na Sanga.

“Sisi tumebakisha mechi moja, tukishinda tunasonga mbele, hilo kombe lingine la mbuzi tunawaachia” alisema Rage.

Katika kuonesha kukerwa kwake na kauli hiyo ya Rage, Sanga ameandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa kueleza: “Ligi Kuu Tanzania bara sio LIGI YA MBUZI, hii ndio ligi inayowafanya Simba wacheze CCL na shirikisho,”

“Hii ndio ligi ambayo serikali na sekta binafsi wamewekeza fedha na kuajili maelfu ya watanzania”

“Hii ndio ligi ilikufanya RAGE uitwe RAGE nchi hii,”

“TUJIZUIE KUROPOKA, PERIOD” Alisema Sanga”

SOMA NA HII  BAADA YA MANARA KUENDELEA KUICHARURA SIMBA...SIMBA SC WAIBUKA NA KUTOA TAMKO HILI