Home Burudani MANULA NA FEI TOTO ‘WATOBOA’ NA Infinix….ISHU NZIMA IKO NAMNA HII…

MANULA NA FEI TOTO ‘WATOBOA’ NA Infinix….ISHU NZIMA IKO NAMNA HII…

Habari njema kwa vijana wapenda soka na wateja wa simu kali za Infinix. Kampuni ya simu Infinix imewatambulisha Rasmi Feisal Salum almaarufu ‘Fei Toto’ anaekipiga katika Club ya YANGA na Aishi Manula kipa wa Simba kuwa mabalozi wa Promosheni ya PIGA UTOBOE yenye kuwawezesha vijana wa Kitanzania na wateja wa Infinix kujizolea zawadi mbalimbali katika msimu huu wa Sikukuu ya Chrismass na Kombe la Dunia kwa kushiriki challenge mbalimbali kupitia @infinixmobiletz na kushinda zawadi kama Fridge, Smart TV na Pikipiki.

Vile vile katika msimu huu wa Chrismass na Kombe la dunia kupitia promosheni ya PIGA UTOBOE Infinix imeanza rasmi kufanya punguzo la bei kwa simu aina ya Infinix HOT 12 play kwa sasa inapatikana kwa bei ya jikoni kabisa na punguzo hili limeanza rasmi kwa simu zote fika katika maduka yao kwani offer ni nyingi sana.

Afisa Uhusiano Infinix Eric Mkomoye amedai kuwa Feisal na Aishi ni mabalozi wa kampeni hii sababu Infinix inathamini kijana mwenye kujituma kupitia kipaji na kupitia Feisal na Aishi tunaamini vijana wengi wataTOBOA kupitia mbinu hizi;

  • Kupitia kipaji chako, onyesha ufundi wa kupiga danadana kisha post na @infinixmobiletz na #PIGA UTOBOE na hapo utakuwa umejiweka kwnye nafasi yakujishindia Infinix NOTE 12.

  • Tembelea @infinixmobiletz bofya link kwenye BIO na utabiri mshindi wa kila mechi ya world cup na ushinde simu.

  • Nunua Infinix NOTE 12, ZERO ULTRA, HOT 12 na ujishinde fridge, TV inch 65, Pikipiki na GB 96 za internet na dakika 2400 za maongezi kuzawadiwa papo hapo kwa mteja wa ZERO ULTRA.

Kila week Infinix itatangaza washindi wa promosheni hii ambayo imeanza rasmi Novemba 19 hadi January 4, usicheze mbali na page ya @infinixmobiletz niwakati wako sasa PIGA UTOBOE

Piga 0712602970 kwa huduma ya haraka.

https://youtu.be/jQoNOZpn27M

 

SOMA NA HII  KISA USHINDI WA YANGA JANA...NCHI NZIMA YATETEMA....MO DEWJI ASHINDWA KUJIZUIA...