Home Uncategorized AZAM FC YAFICHUA KILICHOWAPA USHINDI WA MABAO 3-1 MBELE YA FRIEND RANGERS

AZAM FC YAFICHUA KILICHOWAPA USHINDI WA MABAO 3-1 MBELE YA FRIEND RANGERS

IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kikubwa kilichowapa ushindi mbele ya Friend Rangers ni kucheza kwa nidhamu kwa wachezaji pamoja na kufuata maelekezo.

Azam ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho, jana Januari, 27 waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Friend Rangers mchezo wa hatua ya 32 bora na kwa ushindi huo wametinga hatua ya 16 bora.

“Wachezaji wanapaswa pongezi walipambana mwanzo mwisho kutafuta matokeo na walichokitaka wamekipata, kufuata maelekezo na nidhamu vimewasaidia kutimiza majukumu yao,” amesema.

Azam FC itacheza na Ihefu FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwenye mchezo wake wa hatua ya 16 bora.

SOMA NA HII  BEKI MPYA SIMBA AJA NA KITISHO YANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here