Home Simba SC SportPesa YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KWA SIMBA

SportPesa YAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 50 KWA SIMBA


 KAMPUNI ya burudani na michezo SportPesa jan Mei 27 imekabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 50 kwa timu ya Simba baada ya kufuzu hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya CAF ikiwa ni bonasi kwa hatua waliyofikia.

Hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za SportPesa ambao ni wadhamini wakuu maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam.

 Waliohudhuria kutoka SportPesa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, kutoka Simba ni Mkurugenzi Mtendaji, (CEO) Barbara Gonzalez, Ofisa Habari wa Simba. Haji Manara, benchi la ufundi na baadhi ya wachezaji.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, SportPesa Tarimba Abbas alianza kwa kuwapongeza wachezaji na viongozi wa Simba kwa hatua waliyofikia.

“Nawapongeza viongozi na wachezaji wa Simba SC kwani mmewapa heshima kubwa wana msimbazi kote nchini na kubwa zaidi ni heshima mliyotupa sisi kama wadhamini wenu wakuu kwa mafanikio makubwa na kupambana mpaka kufikia hatua hii.


“Hii ni ishara nzuri kwa mashindano yajayo kwani mtashiriki kwa kujipanga ili kutimiza lengo lenu kama timu.

Aliendelea kwa kufafanua kuhusu kiasi hicho cha pesa ambacho SportPesa imekabidhi kwa Simba kwa kusema;-“Simba imeitendea haki nembo yetu SportPesa na kampuni inaamini sisi kama wadhamini wakuu imekuwa ni moja ya chachu iliyosababisha Simba Sports Club kufuzu hatua hii.

“Tunachokifanya leo ni kutimiza moja ya ahadi tuliyotoa wakati tunasaini mkataba wa udhamini mwaka 2017 kuwa tutatoa bonasi ya Shilingi Milioni 50 endapo mojawapo ya timu tunazozidhamini itafuzu katika hatua ya robo fainali kwenye kombe la shirikisho la mabingwa Afrika,” .


SOMA NA HII  KUHUSU BANGO LA 5G LA YANGA....SIMBA WAAMUA KUCHUKUA HATUA HIZI MAPEMAA...