Home Habari za michezo TABIA YA KUTUKANA TUKANA WATU YAMTOKEA PUANI AUSSEMS…

TABIA YA KUTUKANA TUKANA WATU YAMTOKEA PUANI AUSSEMS…

Habari za Michezo

Shirikisho la Kandanda nchini Kenya FKF limeanzisha uchunguzi dhidi ya kocha mkuu wa AFC Leopards Patrick Aussems kufuatia lugha ya matusi kwa mwandishi wa habari pamoja na kuwaita maofisa KPL kuwa vichekesho.

Aussems ambaye ni kocha wa zamani wa Simba ya Tanzania alisema maneno hayo baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya KPL dhidi ya Nzoia Sugar uliomalizika kwa sare tasa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari alimuita mwandishi mmoja aliyemuuliza swali kuwa ni ‘mpuuzi’ na kuwaita maofisa wa mchezo huo kwamba wamechezesha kama vituko “wanachekesha”.

Afisa habari na masoko Pharis Kimaru alisema shitaka hilo limefika kwenye kamati ya nidhamu ya FKF.

“Tunakuja na maamuzi sawa na kitendo chake, uchunguzi ukikamilika ndani ya siku chache zijazo”, alisema Mtendaji Mkuu wa shirikisho la soka nchini humo Barry Otieno.

SOMA NA HII  SIKU KADHAA TOKA AJIUNGE NA SINGIDA BIG STARS...NDEMLA AIBUKA NA HAYA MAPYA...AGUSIA ISHU YA USAJILI ....