Home Habari za michezo KISA USHINDI WA YANGA JANA…NCHI NZIMA YATETEMA….MO DEWJI ASHINDWA KUJIZUIA…

KISA USHINDI WA YANGA JANA…NCHI NZIMA YATETEMA….MO DEWJI ASHINDWA KUJIZUIA…

Habari za Yanga SC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ameitumia salamu za pongezi klabu ya Yanga kwa kuingia Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Pongezi za dhati kwa Klabu ya Yanga kwa kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup). Mmeandika historia na kuipa nchi yetu heshima kubwa sana. Nawatakia kila la kheri katika mchezo wenu wa Fainali,” amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Tayari Yanga imevuna jumla ya Sh. Milioni 40 katika mfuko wa hamasa wa Rais Samia kutokana na mabao manne waliyofunga kwenye mechi mbili za Nusu Fainali dhidi ya Marumo Gallants.

Yanga imeitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, ikishinda 2-0 nyumbani na 2-1 ugenini jana na kwenye Fainali itakutana na USM Alger iliyoitoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast baada ya sare ya 0-0 ugenini na ushindi wa 2-0 nyumbani.

Yanga itaanzia nyumbani katika Fainali ya kwanza Mei 28 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Algeria kwa mchezo wa marudiano Juni 3 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers.

Aidha kwa upande mwingine, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Yanga kwa ushindi walioupata dhidi ya Timu ya Marumo Gallants na kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Sasa katika kuwapa hamasa Timu ya Yanga Rais Samia amesema atanunua kila goli kwa Tsh Milioni 20 iwapo wataibuka na ushindi katika michezo ya Fainali.

Akizungumza leo Alhamis katika hafla ya uzinduzi wa minara 21 ya kurushia matangazo ya televisheni ardhini (DTT), Rais Samia amesema;

“Tunapokwenda kwenye Fainali, ni miloni 20 kwa kila goli Timu inapotoka na ushindi sio ile wamefungwa mbili halafu wao wakafunga moja hapana”

Rais Samia aliahidi kuniunua kila goli kwa milioni 5 michezo ya Hatua ya makundi, Milioni 10 kwa kila goli hatua ya Robo Fainali na Nusu Fainali na sasa hatua ya Fainali imeahidiwa milioni 20 kwa kila goli timu inapoibuka na ushindi.

Kwa upande mwingine pia Mwekezaji kutoka katika Klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji ameipongeza Klabu ya Yanga baada ya kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Yanga wameingia hatua ya Fainali baada ya kufanikiwa kuiondoa Timu ya Marumo Gallants kwa jumla ya mabao 4-1.

Kupitia Ukurasa wake wa Twitter, Mo Dewji ameandika;

“Hongera sana mtani, you have made Tanzania proud!”

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKIJARIBU KUJIPANGA UPYA..UKWELI KUHUSU YANGA KUWA BINGWA MSIMU HUU UKO HIVI...