Home Habari za michezo MANARA : TUNAWAHESHIMU SIMBA..WANATIMU NZURI NA WACHEZAJI WAZOEFU..LAKINI…..

MANARA : TUNAWAHESHIMU SIMBA..WANATIMU NZURI NA WACHEZAJI WAZOEFU..LAKINI…..


MSEMAJI wa klabu ya Yanga,Haji Manara amesema anawaheshimu Simba kutokana ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu.

Manara alisema hayo jana wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha kuelekea katika mchezo wao ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Simba utakaochezwa Aprili 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Msemaji huyo amesema wanakwenda kucheza mechi wakiwa wanawaheshimu Simba huku akiweka sababu ya pili wametoka kucheza kombe la Shirikisho.

“Wana wachezaji wenye uzoefu, wachezaji wenye uwezo wa kucheza mechi kubwa, ukitoa heshima kwa mpinzani wako na ukashinda basi inakuwa rahisi sana kutamba,” amesema Manara.

Manara aliendelea kutamba akisema msimu huu wamekuwa bora hivyo anaamini kabisa watapata pointi tatu katika mchezo huo.

“Msimu umekuwa mzuri kwetu na tumewafunga Azam kotekote, Mkwakwani tumeshinda na tumewafunga Namungo, Ngao ya Jamii tumewafunga Simba kwahiyo sisi ni bora,” amesema Manara.

Manara alitangaza viingilio vya mchezo wao na Simba jni kuanzia shilingi Elfu 5000 mzunguko, Elfu 10000 (Orange), Elfu 15000 (Vip C), Elfu 20000 (VIP B) na VIP A kwa Elfu 30000.

SOMA NA HII  PAMOJA NA YANGA 'KUSHINE' ....SIMBA NAO WAKO NJEMA AISEE...MAMBO HAYA YAMEWAPA HESHIMA CAF...