Home Uncategorized KAGERE ALETA HOFU SIMBA, STRAIKA MPYA KUTANGAZWA

KAGERE ALETA HOFU SIMBA, STRAIKA MPYA KUTANGAZWA


Wakihesabu saa kabla ya usajili wa dirisha dogo kufungwa hapo jana, inaelezwa viongozi wa Simba wapo kwenye mipango kabambe ya kuhakikisha wanasajili straika mwingine wa kimataifa mwenye uwezo wa kufunga mabao zaidi ya Mnyarwanda, Meddie Kagere.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo ilikose Kombe la Mapinduzi ambalo lilikwenda Mtibwa Sugar baada ya kuwafunga Simba bao 1-0 ambalo lilifungwa na Awadh Juma.

Timu hiyo hadi hivi sasa tayari imefanikiwa kumsajili kiungo mshambuliaji raia wa Msumbiji, Luiz Miquissione aliyekuwa anakipiga UD Songo kwa mkopo akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, viongozi hao wameingia hofu juu ya uwezo wa Kagere katika michezo ya hivi karibuni ukiwemo ule wa watani wa jadi, Yanga na Mtibwa ukitaka kufunga usajili na mshambuliaji matata mwenye uwezo wa kufunga mabao.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa upo uwezekano mkubwa wa Simba leo Jumatano kufunga usajili na mshambuliaji mmoja wa kimataifa mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao kabla ya dirisha kufungwa saa sita usiku baada ya kuamini kuwa Kagere anachoka kutokana na kutumika mara nyingine.

“Ukiangalia uwezo wa Kagere umeshuka kwa kiasi kikubwa na uongozi unaona ni kutokana na kutumika sana katika mechi ambazo wamezicheza hivyo anahitaji kupumzika.

“Ukiachana na Kagere, Bocco naye ambaye ni kati ya washambuliaji tegemeo bado hajawa fiti kwa asilimia kubwa licha ya kupona hivyo ni ngumu kumtegemea ni lazima wasajili mshambuliaji mwingine wa kimataifa atakayekuja kuchukua nafasi ya Wilker Da Silva, aliyesitishiwa mkataba hivi karibuni.

“Hivyo, upo uwezekano mkubwa kesho (leo), kabla ya dirisha la usajili halijafungwa Simba wakafunga usajili na mshambuliaji mmoja wa kimataifa kutoka nje ya nchi lakini pia inaelezwa kuwa wametishwa na kiwango cha Yanga cha sasa,” alisema mtoa taarifa huyo.

Mtendaji Mkuu (C.E.O), wa timu hiyo, Senzo Mazingisa hivi karibuni alisema kuwa timu hiyo ipo kwenye mipango ya kusajili wachezaji katika dirisha dogo kama kocha akitoa mapendekezo.

CHANZO: CHAMPIONI
SOMA NA HII  CORONA YAIVURUGAVURUGA KABISA MBAO FC