Home Uncategorized CORONA YAIVURUGAVURUGA KABISA MBAO FC

CORONA YAIVURUGAVURUGA KABISA MBAO FC


UONGOZI wa Mbao FC umesema kuwa umesitisha program zote kwa sasa kutokana na kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
Janga la Corona limeivuruga dunia kwa kusababisha mambo mengi kusimama ambapo kwenye sekta ya michezo, ligi ya Bongo ilisimamishwa tangu Machi 17.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njash alisema kuwa hakuna kinachoendelea kwa sasa ndani ya klabu yao kutokana na Corona.
“Hakuna kinachoendelea kwa sasa kwani mambo hayaeleweki na upepo wenyewe ndo hivyo tena mambo hayaendi kabisa,” alisema Njash.
Mbao FC ipo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 29.
SOMA NA HII  NYOTA BURUNDI AIPA TANO YANGA USAJILI WA NTIBAZONKIZA