Home Simba SC GOMES ATAJA MBADALA WA WAWA NA LWANGA NDANI YA SIMBA

GOMES ATAJA MBADALA WA WAWA NA LWANGA NDANI YA SIMBA


LEO Machi 16, Didier Gomes, Kocha Mkuu wa Simba atakiongoza kikosi chake kusaka pointi tatu mbele ya Al Merrikh ya Sudan kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya makundi.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Al Hilal, ubao ulisoma Al Merrikh 0-0 Simba hivyo mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Wakati Simba ikiingia Uwanja wa Mkapa bila ya mashabiki pia Gomes atakosa huduma ya beki kisiki Pascal Wawa ambaye ana kadi mbili za njano pamoja na kiungo mkabaji Thadeo Lwanga.

Gomes ameweka wazi kuwa bado ana wachezaji wengi ambao anao na anaamini kwamba watafanya vizuri kwenye mchezo wa leo.

“Ukiangalia kwa upande wa beki wa kati yupo Peter Muduhwa ambaye ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa, anaweza kucheza pia beki wa kati kwa kuwa amekuwa na uelewano mkubwa na Wawa pamoja na Joash Onyango.

“Katika eneo hilo pia yupo Kenedy Juma, Ibrahim Ame hawa wanaweza kufanya kazi hiyo kwa ukamilifu.

“Kwa upande wa kiungo mkabaji ninaweza kubadili mfumo lakini kwenye mechi iliyopita alicheza Mkude, (Jonas) yupo pia Erasto Nyoni hivyo bado kuna namna ya kufanya,” amesema.

SOMA NA HII  MKUDE JONAS, MORRISON WAPIGWA BITI SIMBA NA GOMES