Home epl LIVERPOOL YASEPA NA POINTI TATU ZA WOLVES

LIVERPOOL YASEPA NA POINTI TATU ZA WOLVES


DIOGO Jota nyota wa kikosi cha Liverpool alifunga bao pekee lililoipa pointi tatu muhimu timu yake mbele ya Wolves jambo lililomfurahisha Kocha Mkuu, Jurgen Klopp.

Uwanja wa Molineux bao hilo lilipachikwa dakika ya 45+2 liliwafanya waende mapumziko wakiongoza na kipindi cha pili walilinda bao hilo mpaka zilikamilika dakika 90.

Jota amewamaliza mabosi wake wa zamani, Wolves inayonolewa na Kocha Mkuu, Nuno Santo baada ya kupiga shuti lililomshinda mlinda mlangoRui Patricio kwa kuwa ulikwenda kugonga pembeni ya nguzo na kuzama nyavuni.


Liverpool inafikisha pointi 46 ikiwa imecheza jumla ya mechi 29 na Wolves ina pointi 35 ipo nafasi 13 baada ya kucheza mechi 29 pia.

SOMA NA HII  MBALI NA KICHAPO,MASTAA PSG WALIVAMIWA NA MASHABIKI