Home Habari za michezo KISA KUFUNGA….’MZUNGU’ WA SIMBA AFUNGUKA JINSI ALIVYOPAMBANA NA MASHABIKI INSTGRAM…’WALIKUWA WANASUMBUA’….

KISA KUFUNGA….’MZUNGU’ WA SIMBA AFUNGUKA JINSI ALIVYOPAMBANA NA MASHABIKI INSTGRAM…’WALIKUWA WANASUMBUA’….


Mshambuliaji mpya wa Simba SC Dejan Georgijevic amesema baada ya kufunga bao lake la kwanza dhidi ya Kegera Sugar juzi Jumamosi (Agosti 20), anaamini ataendelea kufanya hivyo kadri atakapopewa nafasi ya kucheza na Kocha Mkuu Zoran Maki.

Dejan aliifungia Simba SC bao la pili kwenye mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku bao la kwanza katika mchezo huo likifungwa na Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Moses Phiri.

Mshambuliaji huyo kutoka Serbia amesema kabla ya mchezo wa juzi, alikua anatamani kuisaidia sana timu yake kufunga na alijitahidi sana kujiandaa akiwa mazoezini.

Amesema alitamani kufanya hivyo ili kujiongezea morari ya kupambana kwa nguvu akiwa katika mazingira mapya ya soka lake, kwani hii ni mara yake ya kwanza kucheza soka katika bara la Afrika.

“Nilikua natamani kufunga ili kutengeneza hali ya kujiamini na morarli kuongezeka kwangu, kwani naamini katika ubora wangu ninao uwezo wa kufunga mfululizo ila kutokana na mazingira ya ugenini lazima nikubali kukabiliana nao.”

“Tangu nilipotambulishwa Simba SC nimekua nikipokea ujumbe kwa lugha ya kiswahili kutoka kwa Mashabiki wengi kupitia Instagram, tofauti na ilivyokua awali, wengi walinihiza kupambana ili niweze kuisaidia timu kufunga.”

“Kuna wakati nilipata muda wa kuchukua baadhi ya ujumbe na kuutafsiri kwa lugha yangu, ndipo nilielewa nini wanachokihitaji kutoka kwangu, nilibaini walikua wanataka kuona nikiisaidia timu kwa kufunga mabao, hivyo kuanza kwangu kufunga ninaamini mambo mengi yatakuja.” amesema Dejan

Dejan alisajiliwa Simba SC akitokea NK Domzale ya nchini kwao Serbia, kwa pendekezo la Kocha Mkuu Zoran Maki ambaye amekua akisisitiza kuamini uwezo wa Mshambuliaji huyo.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA SIMBA...MKWASA AINGIA UBARIDI...ADAI WATAKUWA WAMECHOKA MNOOO...