Home Uncategorized AZAM FC: BADO HATUJAJUA HATMA YA LIGI ITAKUAJE

AZAM FC: BADO HATUJAJUA HATMA YA LIGI ITAKUAJE

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa bado haujajua hatma ya Ligi Kuu Bara kwa sasa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Azam ipo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 28 kibindoni imejikusanyia pointi 54 huku kinara akiwa ni Simba mwenye pointi 71 akiwa amecheza pia mechi 28.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin amesema kuwa bado mambo hayajawa sawa kutokana na Virusi vya Corona.

“Kwa sasa mambo bado ni magumu ukizingatia kwamba kuna hali ya taharuki kuhusu hili janga, hakuna ambaye anajua hatma ya ligi itakuaje ni suala la kuendelea kusubiri na kuomba heri,” amesema.

SOMA NA HII  BREAKING: YASSIN MUSTAPHA ASAINI YANGA KUTOKA POLISI TANZANIA