Home Uncategorized KAHEZA: BADO NAJIFUA NA KUCHUKUA TAHADHARI PIA

KAHEZA: BADO NAJIFUA NA KUCHUKUA TAHADHARI PIA


MARCEL Kaheza, mshambuliaji wa Polisi Tanzania amesema kuwa kwa sasa anaendelea na program maalumu ili kulinda kipaji chake kuwa bora.

Kaheza akiwa ndani ya Polisi Tanzania ametupia mabao saba na ana pasi tano za mabao mguuni mwake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kaheza amesema kuwa amekuwa akifanya mazoezi ili kujilinda kubaki kwenye ubora wake.

“Mazoezi kwangu ni muhimu na programu ambayo tumepewa ninaifuata kwani wakati huu ni muhimu kujilinda na kuchukua tahadhari pia kujilinda na Virusi vya Corona,” amesema.

Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na ligi nyingi duniani zimesimama ili kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona.

SOMA NA HII  ALGERIA BINGWA MPYA WA AFRIKA, AMNYOOSHA SENEGAL KIDOGO TU