Home Uncategorized KOCHA LIGI KUU AWAPA MAJUKUMU YA KUWA MABALOZI WACHEZAJI WAKE

KOCHA LIGI KUU AWAPA MAJUKUMU YA KUWA MABALOZI WACHEZAJI WAKE

JACKSON Mayanja aliyekuwa Kocha Mkuu wa KMC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara amesema kuwa kuna umuhimu wa wachezaji kuchukua tahadhari wakiwa nyumbani kipindi hiki kigumu cha kupambana na Virusi vya Corona.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mayanja ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya KFC ya Uganda inayoshiriki Ligi Kuu ya Uganda amesema afya ya kila mmoja ina umuhimu kuliko michezo.
“Wachezaji wote wakiwa nyumbani wanatakiwa kuwa mabalozi wazuri hasa kwa wakati huu wa maambukizi ya Virusi vya Corona kwani afya ni muhimu kuliko michezo.
“Iwapo watakuwa salama na kizazi chao pia kitakuwa salama kwani watarejea kwenye majukumu yao itakuwa rahisi kuendelea kuwa bora kuliko wakipuuzia na kufanya yale yasiyo ya afya,” amesema.

Mayanja alikiongoza kikosi hicho kutoka kwenye nafasi ya 16 hadi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uganda ana tuzo ya Kocha Bora kwa mwezi Februari.
SOMA NA HII  HIKI HAPA ANACHOKIFANYA ABDI BANDA KULINDA KIPAJI CHAKE