Home Uncategorized JAMES KOTEI:NINAWEZA KURUDI SIMBA

JAMES KOTEI:NINAWEZA KURUDI SIMBA


JAMES Kotei, kiraka wa zamani wa Simba amesema kuwa iwapo mabosi wake wa zamani watahitaji saini yake hana tatizo nao kwani hawakuzinguana.

Nyota huyo kabla ya kusepa ndani ya Simba aliibuka kuwa kiungo bora wa timu kwa msimu wa 2018/19 walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

“Ubora wa Simba hakuna ambaye anaweza kugoma kufanya kazi kutokana na ushirikiano uliopo na ukizingatia kwamba sikugombana na viongozi.

“Iwapo itatokea kila kitu kimekwenda sawa nitarudi kuvaa jezi ya Simba kazi yangu ni mchezaji sichagui kambi,” amesema. 

 Baada ya kusepa Simba aliibukia Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa sasa anakipiga ndani ya Belarus.

SOMA NA HII  WAKATI WA KUWATAMBUA WALIOKUWA WANALETA UJANJAUJANJA LWENYE MAZOEZI UNAWADIA