Home Uncategorized KIUNGO WA MTIBWA SUGAR ANAYEWINDWA NA YANGA AFUNGUKIA ISHU YAKE

KIUNGO WA MTIBWA SUGAR ANAYEWINDWA NA YANGA AFUNGUKIA ISHU YAKE

ABDULHAMAN Humud, kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya Mtibwa Sugar amesema kuwa iwapo Yanga itahitaji saini yake hana tatizo nao lazima atasaini iwapo watafikia makubaliano.

Humud amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ndani ya Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya 14 baada ya kucheza mechi 29 na kwenye mabao 22 waliyofunga yeye amefunga mabao mawili.

Kiungo huyo amesema:”Mchezaji kazi yake ni kucheza bila kujali anacheza wapi lakini kikubwa ni maslahi yake na kujua kile ambacho anakihitaji ni nini kwenye hiyo timu.

“Ishu ya kutua Yanga bado haijawa sawa kwani nami ninaskia tu lakini ikitokea wakafuata taratibu zote sina tatizo katika hili nitacheza bila mashaka,” amesema.

SOMA NA HII  HUYU HAPA NYOT WA AZAM FC AMEPEWA JUKUMU LA KUIMALIZA YANGA LEO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here