Home Uncategorized KINARA WA UTUPIAJI BONGO ATAJA KINACHOWAPONZA WAZAWA KUTUSUA

KINARA WA UTUPIAJI BONGO ATAJA KINACHOWAPONZA WAZAWA KUTUSUA


MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa wazawa wana uwezo mkubwa wa kucheza nje ya nchi ila wanashindwa kujiamini na kujituma ndani ya uwanja.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara ikiwa imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona, Kagere ametupia mabao 19 akiwa ni namba moja kwa utupiaji.

Kagere amesema:” Wachezaji wazawa hasa kwa nafasi ambayo ninacheza ya ushambuliaji wana nafasi ya kufanya vizuri na kuwa bora ila kinachowakwamisha ni kwamba wanashindwa kujiamini na kufanyia kazi makosa yao wanayoyafanya ndani ya uwanja.

“Ikiwa wataongeza juhudi na kufanya kazi kwa kujituma itakuwa rahisi kwao kutusua na kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

“Nafasi yao kwao kutoka nje ipo lakini lazima wasikubali mafanikio ya muda mfupi yatawafanya wasifikie malengo waliyojiwekea,” amesema.

SOMA NA HII  YANGA YAZIMA HUJUMA NA JEURI ZA SIMBA