Home Uncategorized HIZI HAPA DAKIKA 180 ZA MOTO KWA YANGA NA SIMBA KABLA YA...

HIZI HAPA DAKIKA 180 ZA MOTO KWA YANGA NA SIMBA KABLA YA MACHI 8


KUELEKEA kwenye mchezo wa watani wa jadi unaotarajiwa kuchezwa Machi 8, Uwanja wa Taifa wababe hao wamebakiza dakika 180 kabla ya kukutana kwenye mchezo huo.
Mchezo huo Yanga atakuwa mwenyeji ambapo kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa, Januari 4, Simba ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2.
Yanga jana ilikuwa inacheza na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani imebakiza mechi mbili sawa na dakika 180 kabla ya kukutana na Simba ambao nao wamebakiwa na mechi mbili sawa na dakika 180 ambazo ni za ligi.
Februari 29 Yanga itamenyana na Alliance ya Mwanza, Uwanja wa Taifa ikiwa na kumbukumbu ya kusepa na pointi tatu kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba kwa kushinda mabao 2-1 kisha itamalizana na Mbao ambapo mchezo wa kwanza ilishinda bao 1-0.

Kwa upande wa Simba dakika zao 180 walizobakiwa nazo ni mbele ya KMC itakuwa Machi Mosi, Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa kwanza Simba ilishinda mabao 2-0 na Machi 4 itakutana na Azam FC ambapo Simba ilishinda kwa bao 1-0 mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa.
SOMA NA HII  SIMBA KUIFUATA LEO STAND UNITED SHINYANGA