Home Uncategorized KOCHA EVERTON ATAJA SABABU YA KUFUNGWA NA ARSENAL

KOCHA EVERTON ATAJA SABABU YA KUFUNGWA NA ARSENAL


CARLO Ancelotti, Kocha Mkuu wa Everton amesema kuwa kilichowaponza wachezaji wake kupoteza mchezo wao mbele ya Arsenal ni papara na kushindwa kulinda bao lao la kwanza.

Everton kwenye mchezo wa Ligi Kuu England mbele ya Arsenal, Uwanja Emirates walikubali kichapo cha mabao 3-2 licha ya wao kuanza kufunga bao la kuongoza mapema kipindi cha kwanza dakika ya kwanza kupitia kwa Dominic Calvert-Lewin aliyefunga kwa mtindo wa Acrobatic.

Arsenal ilipindua meza dakika ya 27 kupitia kwa Eddie Nketiah na bao la pili lilipachikwa na nahodha wa kikosi hicho, Pierre Emerick Aubameyang aliyefunga mawili dakika ya 33 na 46 bao la pili kwa Everon lilifungwa na Richarlison dakika ya 45.

Ancelott amesema wachezaji wake walijisahau na kushindwa kulinda ushindi wao jambo lililowagharimu. Everton ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 36 na Arsenal ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 37.

SOMA NA HII  KAZE ATUMIA MWAKA MZIMA KUSOMA MBINU ZA JKT TANZANIA