Home Habari za michezo SIMBA WAWAGUSA MKONO WAHANGA WA KATESH….WAMWAGA MISAADA YA MAMILIONI YA PESA…

SIMBA WAWAGUSA MKONO WAHANGA WA KATESH….WAMWAGA MISAADA YA MAMILIONI YA PESA…

Habari za Simba

Simba Sports Club Limited imetoa Mkono wa Pole kwa Watanzania Wenzetu ambao ni Wahanga wa Mafuriko/ Maporomoko ya Udongo yaliyotokea KATESH wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara.

Viongozi wa Klabu ya Simba wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Ndugu Salim Try Again na CEO Ndugu Iman Kajula wametoa msaada huu na kumkabidhi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Ndumbaro akiwepo na Katibu Mkuu wa BMT Dada Neema Kwa niaba ya Serikali katika Kumuunga Mkono Mhe. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan.

Msaada ulitolewa ni Vyakula pamoja na Sukari, Unga wa Ngao, Mafuta na Maji ambavyo vinapelekwa moja kwa moja kwa Waathirika wa Mafuriko/ Maporomoko ya Udongo.

Janga hili ni kubwa kwa Taifa letu maana Tumepoteza Nguvu Kazi kubwa limepelekea kutokea Vifo, majeruhi kwa Binadamu na Mifugo pamoja na Uharibifu wa Miundombinu ya Barabara na Makazi.

Simba Sports Club inawapa Pole sana Wajanga wote na kuwatakia heri Uponyaji wa haraka kwa majeruhi wote wanaopatiwa matibabu.

SOMA NA HII  SIO POA SIMBA NA MBINU CHAFU ZA WYDAD.....UONGOZI WATIA NENO