Home Habari za michezo KUHUSU ‘UTOTO’ WA BALEKE….BENCHIKHA KAMPA ‘MAKAVU YAKE LIVE’…SAIDO NAYE ATANJWA…

KUHUSU ‘UTOTO’ WA BALEKE….BENCHIKHA KAMPA ‘MAKAVU YAKE LIVE’…SAIDO NAYE ATANJWA…

Habari za Simba

Kocha Mkuu wa Simba SC Abdelhak Benchikha amemtaka Mshambuliaji Jean Baleke, sambamba na wale wa eneo la kiungo kukiwa na Clatous Chama, Saidi Ntibazonkiza, kuongeza kasi.

Ipo wazi kwamba, kwenye mechi nne za Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu 2023/24, Simba SC haijapata ushindi jambo linaloongeza presha kwenye Benchi la Ufundi pamoja na wachezaji kukosa utulivu.

Mechi mbili walizocheza nyumbani, zote walishuhudia wakiambulia sare ya kufungana bao 1-1, ilikuwa dhidi ya Power Dynamo na ASEC Mimosas, huku ugenini wakitoka 2-2 dhidi ya Power Dynamos na 0-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha, amesema kuwa ni muhimu wachezaji wake wote kuwa na kasi kwenye kumalizia nafasi zinazotengezwa na kucheza soka la kuvutia.

“Tunajifunza kutokana na makosa, wachezaji wanajituma kutafuta matokeo lakini kasi inaonekana bado haijawa kubwa, hivyo hilo tunafanyia kazi kuona namna gani tutapata matokeo kwenye mechi zijazo,” amesema Benchikha.

Mchezo ujao wa Kundi B, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, Simba SC itacheza ugenini dhidi ya Wydad Casablanca, Jumamosi (Desemba 9) mjini Marrakesh.

Tayari kikosi cha Simba SC kimeondoka nchini Tanzania kuelekea Morocco leo Jumanne (Desemba 05), kupitia Qatar na kinatarajiwa kuwasili kesho kuendelea na maandalizi kabla ya kuwakabili wenyeji wao Jumamosi.

SOMA NA HII  BARCELONA KUUHAMA UWANJA WA CAMP NOU...SABABU HIZI HAPA...