Home Habari za michezo SHAFII DAUDA ATUPA JIWE LA GIZANI KWA MASTAA HAWA WA SIMBA….

SHAFII DAUDA ATUPA JIWE LA GIZANI KWA MASTAA HAWA WA SIMBA….

Habari za Simba

Kabla ya Dirisha la usajili ambalo wengi wanatamani kuona Simba ikiongeza sura mpya kikosini lakini Je waliopo wanatumika ipasavyo ?

Hao wote ni wachezaji wa Simba SC waliosajiliwa kwenye madirisha tofauti ,wapo Simba kwa vipindi tofauti hadi sasa lakini hakuna aliyewahi kupewa dakika tangu kuanza kwa msimu huu 2023/24

Wanafanya mazoezi na timu kama kawaida, wanasafiri na timu kila inapoenda na kupiga picha timu inapozindua jezi mpya lakini lengo mama la wao kusajiliwa hatuoni wakilitimiza .

Je kiwango ni kidogo au hawaendani na mfumo wa timu ? kama ishu ni kiwango na mfumo wakati wanafanyiwa scout hawakuliona hilo ?

Duchu amezima kwa kiwango cha juu sana pale Geita na baadae Mtibwa lakini amerudi Simba anapiga picha za kuzindua jezi tu .

Mohammed Mussa aliwasha sana visiwani kila mtu akawa na matumaini ,cha ajabu amecheza mechi sio zaidi ya tatu tena ni mwishoni mwa uliopita baada ya hapo anakula mbao ndefu hadi leo.

Mwanuke na wengine wanasajiliwa wakifika wanafia mazoezini wakitoka wanakuwa wachezaji wa kawaida.

Unajiuliza tu kama nguo huna mpango wa kuivaa unainunua ya nini ___?

Napokea ripoti zenu mniambie lini mmewaona wakitwanga hoa tangu kuanza kwa msimu labda nasafiri sana matukio yananipita

SOMA NA HII  IBENGE ALIYEKUWA ANATAJWA KUIBUKIA SIMBA ABWAGA MANYANGA