Home Habari za michezo WYDAD WAANZA KUIFANYIA SIMBA FIGISU….RAIS WAO AJIAPIZA KUMALIZA KAZI MAPEMA TU…

WYDAD WAANZA KUIFANYIA SIMBA FIGISU….RAIS WAO AJIAPIZA KUMALIZA KAZI MAPEMA TU…

Habari za michezo

Klabu ya Wydad Casablanca ya nchini imefanya mabadiliko ya uwanja wa Mchezo wao dhidi ya Simba SC na kuuhamishia mchezo wao wa ligi ya mabingwa Afrika katika jiji la Marrakech katika Dimba la Grand stade de Marrakech.

Wydad wameanza figisu mapema kwa Simba baada ya kukosa alama hata moja kwenye mechi mbili ambazo wameshacheza mpaka sasa huku wakidai kuwa sababu ya kuhamisha kutoka Dimba la Mohammed wa V ni hali ya hewa.

Aidha katika hatua nyingine,Rais wa klabu ya Wydad AC, Said Naciri jana wakati anahojiwa na chombo cha habari LE Matin alisema amewajibika kwa matokeo mabaya ya timu.

“Nimewajibika kwa matokeo mabaya ya Timu yangu na nimefanya kikao na benchi la ufundi pamoja na wachezaji ili kutatua changamoto hii, nilikuwa sihudhurii mechi za timu yangu ila hivi sasa nitafanya vya kutosha na timu yetu itafanya vizuri mechi zijazo.”

Wydad imecheza michezo miwili hadi sasa kwenye kundi B na kuambulia vipigo mechi zote, kunaifanya timu hiyo ishike mkia kwenye msimamo wa kundi hilo likiwa linaongozwa na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Mechi ifuatayo kwa Wydad AC ni dhidi ya Simba SC itakayopigwa nchini Morocco siku ya Jumamosi Disemba 9,2023 mida ya saa 4:00 usiku.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTIMULIWA KIMYA KIMYA YANGA...ZAHERA ALA SHAVU POLISI TZ...