Home news BAADA YA KUSOMEWA HUKUMU NA KUKUTWA HANA HATIA…KABURU AIBUKA NA HILI …

BAADA YA KUSOMEWA HUKUMU NA KUKUTWA HANA HATIA…KABURU AIBUKA NA HILI …


BAADA ya aliyekuwa Makam wa Rais wa klabu ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kuachiwa huru ametoa kauli moja.

Maamuzi hayo yametolewa leo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva amehukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi huku ‘Kaburu’ akiachiwa huru baada ya mahakama hiyo kutomkuta na hatia

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba ambaye amesema hakuna ubishi wowote Dola za kimarekani 300,000 zilikuwa zimeingizwa kwenye akaunti ya Klabu ya Simba kupitia benki ya CRDB ambayo ni mauzo ya mchezaji Emmanuel Okwi.

Akizungumza  kwa mara ya kwanza baada ya hukumu hiyo amesema, anamshukuru Mungu kwa kuwa ndiye muweza wa yote na kila jambo lilitokea kwa mipango yake.

“Namshukuru sana Mungu maana bila yeye mimi siwezi kitu, sina la zaidi ya kumshukuru na kumtukuza,” amesema Kaburu muda mchache baada ya hukumu yao kutoka.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF KESHO KUTWA...MAMELOD WAINGIA UBARIDI KWA YANGA...