Home news BAADA YA KUTUMBULIWA …NDAIRAGIJE AAMUA KUWACHARURA GEITA GOLD FC..

BAADA YA KUTUMBULIWA …NDAIRAGIJE AAMUA KUWACHARURA GEITA GOLD FC..


ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Geita Gold, Etienne Ndayirajige amesema hakustushwa na kufukuzwa kwake kwani maisha ya ukocha ndivyo yalivyo.

Kauli ya Ndayiragije inakuja siku chache baada ya kufutwa kazi na uongozi wa klabu hiyo kutokana na muendelezo mbaya wa matokeo tangu timu hiyo ilipopanda Ligi Kuu Bara.

“Maisha yetu sio ya kudumu, leo unaweza ukawa hapa kesho uko kule, hivyo haijanishangaza sana kwa kilichotokea kwa sababu kwenye soka watu huangalia matokeo mazuri zaidi kuliko uhalisia wa vitu vilivyomo ndani,” alisema.

Kwa upande wa aliyekuwa Kocha Mkuu wa Gwambina FC, Athuman Bilali ‘Bilo’ alisema kuwa uongozi wa Geita ulifanya uamuzi wa haraka kumfuta kazi kocha huyo kwani ni mapema sana kumjadili katika mechi nne tu walizocheza.

“Alianza na ratiba ngumu kwa kupoteza michezo miwili ya mwanzo lakini katika hii ya mwisho amepata pointi mbili ina maana anaimarika, lakini sijui wametumia kigezo gani kumfukuza kwa sababu wachezaji waliopo amewakuta na sio mapendekezo yake,” alisema.

Ndayiragije aliwasili nchini Agosti 22, 2021 na kusaini mkataba wa mwaka mmoja akiiongoza timu hiyo katika mechi saba za michuano yote zikiwemo tatu za kirafiki na nne za ligi.

Katika mechi za kirafiki alishinda moja dhidi ya kagera Sugar, sare dhidi ya Polisi Tanzania na Kagera Sugar huku kwenye mechi za Ligi akipoteza dhidi ya Namungo FC (2-0) kisha kufungwa na Yanga (1-0) na kutoa sare katika michezo miwili kwa kufungana bao 1-1 kwenye mechi za Mtibwa Sugar na Mbeya City huku akikusanya pointi mbili wakishika nafasi ya 13.

SOMA NA HII  SI GOLINI TU....HIVI NDIVYO 'MADEMU' WANAVYOMPAPATIIA MAYELE BONGO...NTIBAZONKIZA AFUATIA...