Home Azam FC LWANDAMINA ‘APIGA MKWARA WA KUFA MTU’ YANGA…..AJITABIRIA MAKUBWA…

LWANDAMINA ‘APIGA MKWARA WA KUFA MTU’ YANGA…..AJITABIRIA MAKUBWA…


KOCHA Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina amesema kwa sasa malengo yao ni kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kuondoshwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Azam imerejea juzi nchini ikitokea Misri ilikofungwa bao 1-0 na Pyramids FC na kuondoshwa kwenye michuano hiyo na imeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa.

“Upungufu uliojitokeza umetupa funzo kuelekea michezo yetu ijayo, naamini kutokana na ushiriki huu tumepata mwanga wa kikosi changu kufanya vizuri,” alisema.

Aliongeza kuwa mchezo wao na Yanga huwa mgumu siku zote ila wamejiandaa vyema kuibuka na ushindi baada ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo uliopita dhidi ya Namungo.

“Ninachokifanya ni kuwapa wachezaji wangu mbinu za kuwa na mwendelezo wa matokeo mazuri, kila timu imejipanga hivyo lazima kukabiliane na changamoto za aina yoyote,” alisema.

Winga mshambuliji wa timu hiyo Idd Seleman ‘Nado’ alisema kuwa kutolewa kwao kumewaongezea ari na hamasa ya kupambana zaidi.

SOMA NA HII  DAKIKA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA SUDAN...MAYELE AFUNGUKA ALIVYOMTAMBIA IBENGE..."NITAMFUNGA TENA"...