Home Habari za michezo KUHUSU KUCHELEWA KWA JEZI MPYA ZA SIMBA…ACHANA NA ‘TANATALILA’…UKWELI UKO HIVI AISEE…

KUHUSU KUCHELEWA KWA JEZI MPYA ZA SIMBA…ACHANA NA ‘TANATALILA’…UKWELI UKO HIVI AISEE…

Jezi Mpya za Simba Kimataifa

Simba walizindua jezi mpya kwa ajili ya mechi zao za Kimataifa Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuanzia hatua ya makundi.

Tangu kuzinduliwa kwa jezi hizo bado kumekuwa na malalamiko kutoka kwa Mashabiki kuhusiana na jezi hizo na upatikanaji wake.

Sasa Kitendawili hicho kimeteguliwa na Meneja wa Habari na ,Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally akizungumza kupitia Wasafi Fm leo Februari 15 amesema;

“Kutokana na sherehe za mwaka mpya China, usafirishaji mizigo ulikuwa wakusuasua ikabidi Vunjabei aende China kuhakikisha Jezi hazichelewi ila zikaja kukwama Ethiopia kwasababu ya Ndege za Mizigo kuchelewa”

“Lakini niwajuze Wanasimba zetu mpya zitaingia nchini siku si nyingi kabla ya Mechi yetu dhidi ya Raja Casablanca” amesema Ahmed Ally

SOMA NA HII  MAMILIONI YAZIDI KUWAMIMINIKIA SIMBA QUEENS...BAADA YA MPUNGA WA CAF...WAONGEZEWA ZINGINE 100...