Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WAMOROCCO…SIMBA WAULINDA USIKU NA MCHANA UWANJA WA MKAPA…ISHU IKO...

KUELEKEA MECHI NA WAMOROCCO…SIMBA WAULINDA USIKU NA MCHANA UWANJA WA MKAPA…ISHU IKO HIVI…

Habari za Michezo

Kipigo cha nchini Guinea ni kama kimewashtua mabosi wa Simba baada ya kuamua kuweka ulinzi mzito kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuelekea pambano lao dhidi ya Raja Casablanca kutoka nchini Morocco.

Wikiendi iliyopita, Simba ilipoteza mchezo wa kwanza wa Kundi C kunako Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya Horoya ya nchini Guinea na kupelekea kushika nafasi ya tatu katika kundi hilo linaloongozwa na Raja Casablanca wakifuatia Horoya, wakati Vipers wakiburuza mkia kwenye kundi hilo.

Simba ambao wanatarajia kucheza mchezo wa pili dhidi ya Waarabu hao wa Morocco, Februari 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

Gazeti la Spoti Xtra ambalo jana Jumatatu liliweka kambi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao ulikuwa unafanyiwa ukaguzi na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Ally Mayay kuelekea katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.

Mbali ya ukaguzi huo, Gazeti la Spoti Xtra limewashuhudia maofisa mbalimbali wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wengine kutoka Bodi ya Ligi wakiwa kwenye ukaguzi sehemu mbalimbali uwanjani hapo.

Mbali ya hao, baadhi ya maofisa wa Simba wanajulikana zaidi kama makomandoo nao wameshaweka kambi uwanjani hapo ambapo wamewekwa kuanzia kwenye geti kuu la kuingilia pamoja na maeneo mengine kwa ajili ya ulinzi kabla ya mchezo huo.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA USAJILI MPYA YANGA...NABI AWEKA MAMBO HADHARANI...CHICO USHINDI BYE BYE...ATOA MASHARTI HAYA...