Home Habari za michezo MAYELE AWACHANA SIMBA, AWATAMANI SIO YANGA

MAYELE AWACHANA SIMBA, AWATAMANI SIO YANGA

Habari za Michezo

Straika wa zamani wa Yanga Fiston Mayele akizunguzia ubora wa timu yake ya zamani Yanga kuwa inazidi kupanda kila siku, mwaka jana walicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika lakini sasa hivi wameingia Makundi baada ya miaka 25 kwa hiyo ni hatua kubwa.

Lakini wakati akiwa anazungumzia ubora wa chama lake la zamani ametupa kijembe kwa wapinzani wake Simba kwamba wamebebwa na kanuni timu inaingia Makundi na haijamfunga mwenziye, wamefuzu kwa kanuni.

“Yanga inakua Kila Siku wanacheza na wanakupa burudani, Simba kwanza wameingia hatua ya makundi kwa goli la ugenini we uliona wapi hiyo?,” amesema Fiston Mayele mshambuliaji wa zamani wa Yanga.

SOMA NA HII  KWANI LIGI INAANZA LINI, YANGA YAMNASA STRAIKA MPYA, YAMTAMBULISHA USIKU