Home Habari za michezo SOKA LA ROBERTINHO SIO POA MCHAMBUZI AFUNGUKA HAYA

SOKA LA ROBERTINHO SIO POA MCHAMBUZI AFUNGUKA HAYA

Habari za Simba

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia EA Radio, Stephen Abissay amesema kuwa soka analofundisha Kocha wa Simba SC, Robertinho ndiyo soka linalotakiwa kwa timu zinazotaka ubingwa.

Stephen amesema hayo kufuatia baadhi ya mashabiki wa Simba kudai kuwa timu yao kwa sasa inacheza soka la hovyo hivyo haiwapi burudani huku baadhi yao wakidai kuwa muhimu ni matokeo.

Simba wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya CAFCL bila kushinda mchezo wowote bali kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya kutoa sare ya 2-2 na Power Dynamos kisha sare ya 1-1 kwenye mchezo wa marudiano.

“Ukiangalia kwenye level za mtoano staili ambayo Robertinho anaenda nayo ndio watu wengi wanacheza hivyo, nimeona Mamelodi alivyotolewa na Wydad.

“Nimeona Wydad walivyocheza ishu haikuwa possession ilikuwa oriented na mbinu tu, nimeona Al Ahly alivyomtwanga Wydad fainali, nimeona Yanga alivyokosa ubingwa kwenye game ya USM Alger, hapa kwa Mkapa possession ilikuwa ya Yanga.

“Yanga walicheza mpira uliokuwa unavutia kabisa, anafika kwenye boksi kama anafunga lakini jamaa wako very compact pale nyuma, ila walitoka mara mbili tu wakawaadhibu Yanga kisha wakarudi.

“Kwa hiyo mpira wa Robertinho utazidi kuwa zaidi ya huu waliouona kwa Power Dynamos kwa sababu approach nyingi zinachezwa hivyo kwenye knock out Stage,” amesema Abissay Stephen.

SOMA NA HII  MAYELE AWEKA REKODI HII YANGA...APEWA JEZI YA HESHIMA...ISHU NZIMA IKO HIVI