Home Habari za Yanga BAADA YA KUIONA RANGI HALISI YA YANGA….STAA WA ZAMANI WA NEWCASTLE YA...

BAADA YA KUIONA RANGI HALISI YA YANGA….STAA WA ZAMANI WA NEWCASTLE YA EPL KAAMUA KUFUNGUKA HAYA YA MOYONI…


Kiungo wa Yanga aliyewahi kukipiga Newcastle United ya Ligi Kuu England, Gael Bigirimana baada ya kupiga tizi la kufa mtu na Wanajangwani hao na kuanza kuzoea mazingira ya Tanzania amesema, “sasa niko tayari kupambana.”

Gael aliyekulia England na kuishi aliwahi kuichezea timu ya taifa hilo chini kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20, kabla ya kubadili mawazo na kuichezea nchi yake ya asili Burundi, ameeleza kuwa tayari kukiwasha Yanga ikiwa ni mara yake ya kwanza kucheza ligi Afrika.

Nyota huyo wa zamani Rangers, Hibernian na Motherwell zote za Scotland amesema wakati anafika Yanga alikumbana na changamoto ya mazingira na pia kuzoeana na wachezaji wenzake, lakini sasa kila kitu kipo freshi na yupo tayari kuleta maufundi ya Ulaya ndani ya Yanga.

“Ni mara yangu ya kwanza kucheza ligi Afrika licha kuwa nimekuwa naitumikia timu ya taifa ya Burundi mara kwa mara, hivyo nilihitaji muda kidogo kukaa sawa.

“Kwa sasa nimeimarika kila idara na kilichobaki ni kuonesha nini nilichonacho na kuisaidia Yanga kufikia malengo yake,” alisema Gael.

Kiungo huyo amekiangalia vyema kikosi cha Yanga na kulinganisha timu nyingine alizowahi kucheza sambamba na za Tanzania akaweka wazi kuwa ni moja ya timu imara.

“Yanga ni timu bora, kuanzia kwa uongozi, benchi la ufundi, wachezaji hadi mashabiki kila mmoja anatimiza majukumu yake ipaswavyo ni miongoni mwa timu chache ulimwenguni zinazofanya hivyo hususani Afrika,” alisema.

Kwa upande wa wachezaji tupo tayari kufanya vizuri na kuwapa furaha mashabiki wetu kwani lengo ni kushinda kila mchezo,” alisema Gael ambaye licha ya Newcastel aliwahi kuzichezea pia Coventry na Solihul Moors zote za England. 

SOMA NA HII  BAADA YA TETESI KUWA NYINGI....OKWA AVUNJA UKIMYA ISHU YA KUTAKA KUACHWA SIMBA SC ....